Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema chini ya uongozi wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli licha ya changamoto mbalimbali lakini waliazimia kufanikisha ndoto ya siku nyingi ya Taifa hili ya kuratibu na kujenga mtradi wa umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kitendo ambacho kiliibua shangwe kwa wananchi waliohudhuria tukio hilo. Rais Samia ameyasema hayo hii leo Desemba 22,2022 mara baada ya kushiriki zoeli la ujazaji maji katika Bwawa hilo huku akiielekeza Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuweka mipango thabiti ya ufugaji wa kisasa wa samaki katika na kwamba kwa kuwa lipo ndani ya hifadhi, uvuvi utakaofanyika ni lazima uwe wa kisasa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema, “Nchi yetu chini ya uongozi wa mpendwa wetu Dkt. John Pombe Magufuli katika awamu ya tano, tukasema liwalo na liwe lakini azma hii ya Mwalimu (Julius K. Nyerere) ya ujenzi wa Bwawa hili la kufua umeme ni lazima tuitekeleze. Kupitia bwawa hil
Kajala Kupelekwa Mahakamani Baada ya Kumtosa Harmonize Kudaiwa Fidia Kwa Makosa Mawili MADAI yanayoendelea mitandaoni kuwa penzi la mwigizaji Kajala Masanja na msanii Rajab Kahali ‘Harmonize limevunjika limekaa vibaya kisheria. Endapo jambo hili ni kweli, Kajala anakabiliwa na hatari ya kupelekwa mahakamani kufunguliwa mashtaka kwa makosa mawili. Kifungu cha 69( 1 ) cha Sheria ya Ndoa iliyofanyiwa marekebisho 2010 kinasema kuwa mtu anaweza kufungua shauri na kudai fidia baada ya uchumba kuvunjwa. Ifahamike kuwa katika siku za hivi karibuni Kajala na Harmonize walijitangaza kuwa ni wachumba baada ya mwanaume huyo kumvisha pete mwanadada huyo, jambo ambalo linawaweka wawili hao katika hatari ya kufikishana kortini kidaiana fidia na zawadi. Kudai fidia na kurudisha zawadi ni vitu viwili tofauti ambavyo vyote vinaweza kumtia mmoja wa wachumba kwenye kasheshe ya kisheria. Kwa tafsiri rahisi fidia inahusu kulipwa maumivu aliyopata mmoja wa wachumba (mume au mke) kutokana na tukio hilo la ku