Urusi imeendelea kutekeleza mashambulio yanayolenga eneo la Kusini Mashariki mwa Ukraine kwa makombora na ndege zisizo na rubani wakati huu pia mataifa ya Magharibi yakithathmini kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Moscow.
Mashambulio hayo yanakuja wakati huu ambapo mamilioni ya watu nchini Ukraine wakiwa bado gizani baada ya makombora ya Urusi kuharibu miundo mbinu muhimu ya nishati wikendi iliyopita.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, katika mazungumzo yake na viongozi wa Marekani, Ufaransa na Uturuki, ametaka vikwazo zaidi kuwekewa Urusi kwa kuendeleza vita vinavyoendelea.
Nao Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, wamekubaliana kuongeza fedha kwa ajili ya Ukraine, kwa zaidia ya Euro Bilioni 2, wakati huu pia ikijadili vikwazo zaidi dhidi ya Moscow.
Haya yanajiri wakati huu huduma zikiwa zimerejelewa katika bandari nyeusi ya Odesa mapema leo baada ya kuwa zimesitishwa baada ya shambulio la Urusi kwa kutumia ndege zisizo na rubani zilizotengenezewa nchini Iran.
Maoni
Chapisha Maoni