Aston Villa yamsajili Mtanzania Mbwana Samatta
Aston Villa inafurahi kutangaza rasmi kumsaini Mbwana Samatta kutoka KRC Genk.Mshambuliaji huyo amemwaga wino kwenye mpango wa miaka minne unusu chini ya idhini ya kibali cha kazi na idhini ya kimataifa.
"Nimefurahi sana," Samatta alisema. "Ni hatua kubwa kwangu katika kazi yangu. Ni hatua kubwa kwa nchi yangu pia. Kila mtu alikuwa akitafuta Mtanzania kucheza kwenye Ligi Kuu za kimataifa hatimaye nimewatoa kimasomaso.
"Ninajua mengi juu ya Aston Villa. Nilikuwa nikitazama rekodi ya Ligi kuu wakati Gabby Agbonlahor alipokuwa hapa."
Mbwana Samatta amefunga mabao 10 kwa timu yake ya awali ya Genk katika mashindano yote msimu huu ikiwa ni pamoja na bao alilolifunga huko Anfield dhidi ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa.
Meneja wa villa Dean Smith alionesha furaha yake baada ya saini kuwekwa ."Nimefurahiya sana tumefanikiwa kumleta Mbwana Samatta klabuni,"
"Amefunga mabao katika kipindi chote cha kazi yake na ninatarajia kufanya kazi naye."
Samatta atakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza kwenye Ligi Kuu lakini hataweza kushiriki kwenye mechi ya nyumbani ya Villa dhidi ya Watford Jumanne.
Villa wamecheza mechi zao tatu za mwisho bila mshambuliaji anayetambuliwa baada ya kumpoteza mchezeshaji wa mbele mwenye asili ya Brazil Wesley kwa msimu wote baada ya kupata jeraha la goti lililodumu huko Burnley Siku ya Mwaka Mpya.
Samatta ndiye mshindi wa tatu kwa timu ya Aston Villa kupata usajili wa dirisha la uhamisho kufuatia saini mbili za mkopo baada ya watangulizi wake kiungo wa kati Danny Drinkwater kutoka Chelsea na kipa Pepe Reina kutoka AC Milan.
Wakati huo huo, kipa wa akiba wa Villa, Lovre Kalinic amejiunga na klabu ya Toulouse ya Ufaransa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Maoni
Chapisha Maoni