RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kufunguliwa kwa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani, kutasaidia kuwaandaa vijana kuwa viongozi wazuri baadaye na kubadilisha mawazo na mitazamo yao ili kuisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo.
Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 23, wakati wa uzinduzi wa chuo hicho kinachomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi CCM ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa vyama sita rafiki vilivyopigania ukombozi katika nchi za Kusini mwa Afrika.
Ameongeza kuwa chuo hicho kitakwenda kufanya kazi ya tathimini ya maendeleo yaliyofikiwa kwenye nchi 6 zilizopigania uhuru katika nchi za kusini mwa Afrika na kwamba na kuangalia mwelekeo wa namna nchi hizo zitakavyosonga mbele kwa pamoja.
Maoni
Chapisha Maoni