Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 24.02.2022:Rice, Kane, Dembele, Isak, Azpilicueta, Johnson, Simon
Manchester United wana uhakika wa kufikia malengo yao ya uhamisho msimu huu wa joto hata kama watashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, huku kiungo wa kati wa West Ham ya Uingereza Declan Rice, 23, na mshambuliaji wa Tottenham, 28, Harry Kane, akiwa kwenye orodha yao. (ESPN)
Chelsea na Paris St-Germain wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake wa Barcelona utakapokamilika msimu huu wa joto. (90min)
Arsenal wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona kumnunua mshambuliaji wa Real Sociedad na Uswidi Alexander Isak, 22, ambaye ni mmoja wa walengwa wakuu wa mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta msimu huu wa joto. (Daily Express)
Barcelona wamempa mlinzi wa Uhispania Cesar Azpilicueta kandarasi ya miaka miwili ili kujiunga na klabu hiyo kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wa mchezaji huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 32 utakapokamilika mwishoni mwa msimu. (Sport - In Spanish)
West Ham wamechagua kuongeza kandarasi ya mlinzi wa pembeni wa Uingereza Ben Johnson,22, hadi mwaka 2024 ili kuzuia uwezekano wa kutakiwa na Arsenal, Tottenham na Liverpool
Spurs wanavutiwa na mlinda mlango wa Athletic Bilbao na Uhispania Unai Simon, 24, huku wakifikiria kuhusu mbadala wa muda mrefu wa Mfaransa Hugo Lloris, 35. (Marca)
Leicester City wanaweza kufufua nia yao ya kumnunua winga wa Italia Domenico Berardi ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ataamua kuondoka Sassuolo inayoshiriki Serie A msimu huu. (Leicester Mercury)
West Bromwich Albion wanamlenga kiungo wa kati wa Uingereza Sean Longstaff, 24, ambaye alicheza chini ya kocha wa Baggies Steve Bruce katika klabu ya Newcastle United. (Football League World)
Mkufunzi wa zamani wa Hull City Grant McCann, 41, amekubali dili la kuwa meneja wa klabu ya Championship Peterborough United. (Football Insider)
Tottenham wako tayari kumuuza Steven Bergwijn msimu huu wa joto huku AC Milan wakimtaka winga huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24. (Calciomercato)
West Ham United inaweza kufikiwa na winga wa Lille Jonathan Bamba, ingawa klabu hiyo ya Uingereza inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Atalanta, Sevilla na Bayer Leverkusen kumnunua Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 25. (Gazzetta dello Sport)
Roma watafufua shauku yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka mwishoni mwa msimu huu licha ya kushindwa katika jitihada za kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi mwenye umri wa miaka 29 msimu uliopita. (Calciomercato - in Italian)
Maoni
Chapisha Maoni