Mzozo wa Ukraine:Putin atangaza operesheni ya kijeshi nchini Ukraine
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza "operesheni ya kijeshi" katika eneo la Donbas nchini Ukraine.
Alitoa tamko hilo katika hotuba ya televisheni huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likimsihi aache.
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni siku ya Alhamisi asubuhi, Putin anawataka wanajeshi wa Ukraine katika eneo la mapigano mashariki mwa Ukraine kuweka silaha chini na kurejea majumbani mwao.
Aliionya Ukraine kwamba italaumiwa kwa umwagikaji wa damu wowote.
Putin pia anasema "haki na ukweli" ziko upande wa Urusi, akionya kwamba jibu la Moscow litakuwa "papo hapo" ikiwa mtu yeyote atajaribu kuchukua dhidi ya Urusi.
Rais wa Urusi pia anasema hatua za nchi yake ni kujilinda na kuwaambia wanajeshi wa Ukraine baba zao na babu zao hawakupigana ili waweze kuwasaidia Wanazi mamboleo.
Rais Zelensky aonya Urusi: Tutajilinda
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky awali alionya kwamba Urusi inaweza kuanzisha "vita vikubw barani Ulaya" siku yoyote sasa, na kuwataka Warusi kuipinga.
Katika hotuba yake usiku wa manane, alisema alikuwa ametafuta mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin bila mafanikio.
"Nilianzisha jitihada za kumtafuta kwenye simu Matokeo: kimya," Bw Zelensky alisema.
Alisema Urusi ina takriban wanajeshi 200,000 na maelfu ya magari ya kivita kwenye mipaka ya Ukraine.
Na kubadilisha kutoka Kiukreni hadi Kirusi, Bw Zelensky alitoa wito kwa Warusi kukataa shambulio, akisema walikuwa wakidanganywa kuhusu Ukraine.
"Ni nani anayeweza kuzuia (vita)? Watu. Watu hawa wako kati yenu, nina hakika," alisema.
Kiongozi wa Ukraine alisema nchi yake iko tayari kwa mashambulizi ya Urusi, na kuapa: "Ikiwa [Urusi] watashambulia, ikiwa watajaribu kuchukua ardhi yetu - uhuru wetu, maisha yetu, maisha ya watoto wetu - tutakuwa tukijilinda."
"Unaposhambulia, itakuwa nyuso zetu unazoziona, sio migongo yetu," rais wa Ukraine alisema.
Ilikuja wakati wanajeshi wa Urusi, walioamriwa kuingia katika mikoa miwili inayodhibitiwa na waasi nchini Ukraine, wakiripotiwa kukaribia mpaka.
Moscow ilisema kuwa mikoa iliyojitenga mashariki mwa Ukraine iliomba msaada wa kijeshi.
Je Putin anataka kufufua Muungano wa Soviet?
Magazeti na tovuti katika nchi za kiarabu zinaendelea kujadili mgogoro wa Urusi na Ukraine na athari za tangazo la rais wa Urusi Vladimir Putin la kutambua uhuru wa mikoa miwili inayodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine, Donetsk na Luhansk.
Mjadala uliegemea kwenye kujiuliza kama lengo la Putin ni kutaka kufufua muungano wa Soviet na kurejesha ushawishi wa Urusi, wakati wengine walizungumzia mgogoro kati ya Putin na nchi za Magharibi, na maoni yaligawanyika kati ya wale ambao waliamini Putin alikuwa hajaeleweka na wale wanaorejelea mgawanyiko hasa nchi za magharibi.
'Kuufufua wa Muungano wa Sovieti"
"Je, Putin anataka kufufua muungano wa sovieti?"
"Rais Vladimir Putin kutambua uhuru wa Donetsk na Luhansk Mashariki mwa Ukraine kulifufua madai ya Magharibi kwamba alikuwa akitafuta "kurejesha muungano wa Soviet," hasa aliposema kwamba "kuanguka kwa muungano wa Soviet ni janga kubwa la kijiografia la karne ya 20."
Magazeti hayo yanaendelea kueleza kwamba ingawa Moscow imekanusha kuwa "imeelezea utofauti wake kuhusu vikwazo vya magharibi."
Katika ukurasa wa maoni, Sobhi Ghandour anasema: "katika miaka iliyopita, siasa za "Putinic" za Urusi hazijarudi kwenye hali ya vita baridi, lakini kwa uimara, inarejesha baadhi ya nafasi za ushawishi ambazo Moscow ilizipoteza kufuatia kuanguka kwa umoja wa Soviet. " Moscow imerudi Mashariki ya kati na sasa ni nchi kubwa yenye uwezo wa misaada na makatazo."
Ujumbe wa Moscow kwa nchi za Magharibi"
Kwenye Bahrain Gulf news, Abdel moneim ibrahim anahoji kuhusu ujumbe ambao Moscow inatafuta kutuma kwa kutambua uhuru wa Jamhuri za Donetsk na Luhansk.
Anasema inataka kutuma "ujumbe wa Urusi kwa Marekani, Magharibi na NATO kwamba Moscow haitaacha ahadi zilizowekwa za kutopanua NATO upande wa Mashariki na kwamba ikiwa hii haitafikiwa kupitia mazungumzo ya kidiplomasia, Moscow ina njia nyingine za kukabiliana na Ukraine na Magharibi."
Al-thidi anaeleza jambo muhimu la mgogoro wa Urusi na Ukrainian, nafasi isiyo ya kawaida ya magharibi.
"Kila mtu anakwepa ukweli, ambao ni kujibu kijeshi, ukiacha maneno ambayo Biden alisema katika mkutano wake jana kwamba atatetea kila inchi ya NATO, hakuna kitu halisi ambacho Putin na serikali ya Urusi wanaweza kuogopa," anasema
Maoni
Chapisha Maoni