Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mzozo wa Ukraine na Urusi: Ukraine yawaambia raia wake waondoke Urusi, huku ikitangaza hali ya dharura

Mzozo wa Ukraine na Urusi: Ukraine yawaambia raia wake waondoke Urusi, huku ikitangaza hali ya dharura

Wanajeshi wa ziada wa ukraine

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa ziada wa Ukraine, wakifanya mazoezi ya kijeshi

Ukraine pia inawakusanya wanajeshi wa ziada pamoja na wanajeshi wake wa kawaida kwa ajili ya kujiandaa kwa uwezekano wa uvamizi

Baraza la kitaifa la usalama na ulinzi la Ukraine linafanya kazi kwa muda wa saa 24 kila siku na katibu wake mkuu amefanya mkutano na waandishi wa habari na kuwaambia kwamba Ukraine imeweka hali ya tahadhari.

'' Hali ya tahadhari itawekwa katika nchi nzima ya Ukraine isipokuwa sehemu ya Donetsk na Luhansk'', amesema.

Haya yanajiri huku, Urusi ikikabiliwa na mfumko wa bei ya mafuta na gesi huku mataifa hususan ya magharibi yakiiwekea vikwazo.

Hali ya tahadhari ina maanisha nini?

Maandalizi ya kwanza yanaendelea katika kile ambacho Rais Zelensky alisema jana katika hotuba yake kwa taifa kwamba ni kuwaita askar iwa akiba.

Ninafahamu kuwa wanaume wengi na wanawake waliitwa leo na kuenda kwenye ofisi za jeshi leo.

Hali ya tahadhari sio sheria ya kijeshi, ambayo pia inaweza kuwekwa katika Ukraine. (kama katibu wa baraza la usalama na ulinzi alivyosema leo ) iwapo uvamizi zaidi utafanyika.

Raia hawataihisi hali ya dharura. Imetolewa kwa mamlaka, haki ya kuwalinda watu wake na utaifa dhidi ya uwezekano wa hatari.

Petrol pump

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Bei ya mafuta na gesi ilipanda Jumanne kwa hofu kwamba mzozo wa Ukraine na Urusi utatatiza usambazaji kote ulimwenguni.

Bei ya mafuta yasiyosafishwa ilipanda zaidi kwa miaka zaidi ya dola 99 (£73) kwa pipa baada ya Rais Vladimir Putin kuagiza wanajeshi kuingia mashariki mwa Ukraine.

Lakini bei baadaye zilidhibitiwa, licha ya nchi za Magharibi kutangaza vikwazo vya kiuchumi na hatua za kuzuia bomba kuu la gesi la Urusi.Hisa pia zilisababisha hasara ya mapema.

Baada ya kushuka kwa zaidi ya asiliamia 1.5 katika biashara ya mapema Jumanne, Wall Street ilirejea shughuli kufuatia matamshi ya Rais wa Merika Joe Biden akielezea majibu ya Marekani. Hisa za Dow zilifunga kwa asilimia 1.4, hata hivyo hisa za S&P 500 zilishuka kwa asilimia 1 huku za Nasdaq zikianguka kwa asilimia 1.2.

Hapo awali, soko la hisa la Japan lilifunga kwa asilimia 1.7 chini, na la China likipungua karibu asilimia 1, huku masoko la hisa huko Ulaya na Uingereza yakifunga .

Maumivu upande wa mafuta

Urusi ni nchi ya pili kwa mauzo ya mafuta nje ya nchi baada ya Saudi Arabia na mzalishaji mkuu wa gesi asilia duniani.

Hatua za kulazimisha nchi kupunguza uzalishaji mafuta yasiyosafishwa au gesi asilia zitakuwa na "madhara makubwa" kwa bei ya mafuta na uchumi wa dunia.

"Uamuzi wa Urusi kuivamia Ukraine tayari unasababisha bei ya mafuta kupanda na bila shaka itasababisha kupanda kwa bei ya mafuta hadi pauni 1.50 kwa lita [ya petroli isiyo na risasi]," kulingana na msemaji wa kampuni ya mafuta ya RAC Simon Williams.

"Hii inaleta habari mbaya kwa madereva nchini Uingereza wanaotatizika kumudu kuweka mafuta kwenye magari yao."

Lakini hatua zilizotangazwa na Marekani, Uingereza na Ulaya kufikia sasa hazifikii kile kilichotishiwa katika tukio la uvamizi.

Vikwazo hivyo vinalenga taasisi za fedha, wasomi na mashirika mengine ya serikali nchini Urusi, kwa sehemu ikilenga kuzuia uwezo wa serikali ya Urusi kukusanya pesa kwenye masoko ya fedha ya Magharibi.

Siku ya Jumanne, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz pia alichukua hatua muhimu ya kuzuia uidhinishaji wa bomba la Nord Stream 2 ambalo lingesambaza gesi moja kwa moja kutoka Urusi hadi Ujerumani.

"Ikiwa Urusi itaendelea zaidi na uvamizi huu, tunasimama tayari kwenda mbali zaidi," Rais wa Marekani Joe Biden alisema katika hotuba yake kutoka Ikulu ya White House.

Pia alionya kuwa kutetea eneo la Nato kunaweza kuwagharimu umma kwa njia ya bei ya juu ya nishati.

A Ukrainian service member uses a periscope while observing the area at a position on the front line near the village of Travneve in Donetsk region

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Tangu mwanzo wa mwezi Februari, bei ya mafuta tayari imepanda kwa zaidi ya asilimia 10 wakati wa mvutano.

Maike Currie, mkurugenzi wa uwekezaji huko Fidelity International, alisema bei ya mafuta inaweza kupanda hadi zaidi ya dola 100 kwa pipa kutokana na mgogoro wa Ukraine, majira ya baridi kali nchini Marekani, na ukosefu wa uwekezaji katika usambazaji wa mafuta na gesi duniani kote.

"Urusi inachangia moja kati ya mapipa 10 ya mafuta yanayotumiwa duniani kote, hivyo ni mhusika mkuu linapokuja suala la bei ya mafuta, na bila shaka, itawaumiza watumiaji kwenye pampu za petroli," alisema.

Mpango wa Urusi kukabiliana na vikwazo vipya

Urusi imetumia miaka mingi kujiandaa kwa wakati huu.

Mnamo mwaka wa 2014, wakati wanajeshi wa Urusi walipohamia Crimea, na kuteka sehemu ya Ukraine, ilizua raundi ya kwanza ya vikwazo vya kimataifa, na hiyo ikawa fundisho muhimu kwa Urusi.

Tangu wakati huo imekuwa ikiweka ulinzi, ikiacha kutegemea dola, na kujaribu kuukinga uchumi wa Urusi kutokana na vikwazo.

Rais Putin anaweza kuwa anaweka dau kuwa anaweza kustahimili vikwazo kwa muda mrefu zaidi ya inavyodhaniwa na nchi za Magharibi.

Sehemu kubwa ya mafuta na gesi ambayo Uingereza inaagiza haitoki Urusi, lakini itaathiriwa na kupanda kwa bei ya kimataifa.

Bei ya wastani ya dizeli nchini Uingereza ilifikia 152.51p kwa lita siku ya Jumatatu, chini ya rekodi ya Jumapili ya 152.58p.

Bei ya jumla ya gesi ya Uingereza pia imepanda, bei ya Uingereza kwa utoaji wa Aprili imeongezeka kwa asilimia 9.

Utegemezi wa kiuchumi kati ya Urusi na Ulaya huenda ukazuia hatua za Magharibi kuendelea, alisema Shaistah Akhtar, mtaalamu wa sheria za vikwazo kutoka kampuni ya sheria ya Uingereza Mishcon de Reya.

Edward Gardner, mchumi wa bidhaa katika Capital Economics alisema mvutano huo huenda ukafanya bei ya mafuta iwe juu, hata kama nchi za Magharibi hazitachukua hatua kali zaidi.

"Si kwa maslahi ya kiuchumi ya Urusi au Magharibi kutumia biashara ya nishati kama silaha dhidi ya kila mmoja, lakini hiyo haimaanishi kuwa haitafanyika," aliandika katika barua Jumanne.

"Hata kama nchi za Magharibi hazitatekeleza vikwazo vya moja kwa moja kwa mauzo ya nje ya nishati ya Urusi, mvutano na Urusi unaweza kuweka bei ya mafuta kuwa juu kwa muda mrefu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HERUFI NA MAANA ZAKE,MAANA YA MAJINA YOTE

A; Haraka, Pupa ya Maisha Wenye jina linaloanza na herufi ”A” ni Watu wanaopenda mambo makubwa, Wanajiamini, na wenye uwezo wa kutimiza malengo yao, Ni watu wenye tahadhari Katika kila jambo, Wachangamfu na wanaopenda Matukio. Wanapenda kuheshimiwa, Wanapenda mamlaka, Wana kiburi na ni Watu wenye hasira. B ; Inawakilisha Kazi, Pesa, Mapenzi, Ujenzi. Wenye jina linaloanza na herufi “B” ni Watu Wakarimu , Waaminifu na Wenye kupenda kazi. Ni watu Jasiri, Shujaa na Wakatili katika vita au pale wanapotaka kulinda vyake au vilivyo katika himaya au Mamlaka yao. C; Inawakilisha Vurugu, Ndugu, Kuchanganyikiwa. Wenye jina linaloanza na herufi “C” ni Watu wa kubadilika badilika, Washindani, na hupenda kupigania Malengo yao wanayoyapenda. Ni watu Wabunifu, na wanaopenda Mawasiliano. D; Inawakilisha Upole, Kuchelewa, Wazee, Cheo. Wenye jina linaloanza na herufi “D” ni Watu wanaopenda Usawa, na Kufanya Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na wenye kupenda Usafi. Ni jeuri na wenye Msimamo. E; Inawa

TMA Yatoa Angalizo La Mvua Kubwa

MAMLAKA  ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa angalizo la mvua kubwa kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, Pwani ikijumuishwa na visiwa vya Mafia, Ruvuma, Morogoro, Njombe, Lindi na Mtwara itakayonyesha hii leo Februari 23, 2022.   TMA imesema kuwa kutakuwa na upepo mkali katika maeneo ya ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, na Tanga.   Aidha, TMA imeongeza kuwa mvua itaendelea kunyesha kwa siku mbili zijazo kwa baadhi ya mikoa nchini Tanzania.

Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa amefariki dunia leo, akiwa na umri wa miaka 81

Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa amefariki dunia leo, akiwa na umri wa miaka 81. Taarifa za kifo chake zimetangazwa kwa taifa usiku wa kuamkia leo Ijumaa kupitia televisheni na Rais John Magufuli kutokea mji mkuu Dodoma. Katika taarifa hiyo, Rais Magufuli amesema, “ndugu zangu watanzania, habari za jioni na habari za usiku. Usiku wa kuamkia leo kwa sababu sasa ni saa 6 karibu na dakika 25, kwa masikitiko makubwa tumepata msiba mkubwa. Mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais wa awamu ya Tatu, amefariki. Amefariki kwenye hospitali Dar es salaam ambako alikuwa amelazwa, niwaombe watanzania tulipokee hili na tumepata msiba mkubwa na tuendelee kumuombea mzee wetu, Rais mstaafu Benjamin William Mkapa, ambaye ametangulia mbele ya haki. Taarif azinigne zitaendelea kutolewa lakini Mzee Mkapa hatunaye tena, asanteni sana.”  Kufuatia kifo hicho, serikali ya Tanzania imetangaza siku 7 za maombolezo ambapo bendera itapepea nusu mlingoti. Rais mstaafu Mkapa ambaye alizaliwa tarehe 12

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 07.02.2020: Pogba, Traore, Martinez, Smalling, Piatek

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 07.02.2020: Pogba, Traore, Martinez, Smalling, Piatek 7 Februari 2020 CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Paul Pogba Manchester United wamepunguza dau la kumuuza kiungo wao nyota Paul Pogba, 26, kwa pauni milioni 30. Sasa United watakubali kumuuza Mfaransa huyo kwa pauni milioni 150. (Sun) Pogba ameondolewa kwenye msafara wa Manchester United nchini Uhispania. (Star) Barcelona wanajipanga kumsajili winga wa Wolves Adama Traore, 24, mwishoni mwa msimu huu. (Mail) CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Adama Traore Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anapanga kukisuka upya kikosi cha kwanza cha Gunners ambapo anatarajiwa kuwauza mshambuliaji wa Gabon striker Pierre-Emerick Aubameyang, 30, mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 28 na kiungo Mjerumani Mesut Ozil, 31. (Sun) MATANGAZO Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22, anajiandaa kuzikacha klabu za Man United na Man City mwishoni mwa msimu ili ajiunge na vigogo w

Mama amzika mwanawe akiwa hai ili akajiuze

​Mama amzika mwanawe akiwa hai ili akajiuze Geita. Mkazi wa Buseresere wilayani Chato mkoani Geita, Oliva Meshack anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumzika mwanae wa wiki mbili akiwa hai ili apate muda wa kwenda kujiuza. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 19 anadaiwa kutenda kosa hilo kabla ya majirani kumtilia shaka na kuripoti kituo cha polisi. Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amewaeleza waandishi wa habari leo Desemba 15, 2022 kwamba tukio hilo limetokea na lilibainika baada ya majirani kutoa taarifa polisi. “Jeshi la polisi lilipata taarifa kwa wananchi kuwa kuna binti aliyejifungua lakini wana siku tatu hawamuoni binti na mtoto na wakataka kujua alikopeleka mtoto, tulimchukua binti na kumhoji na alikiri alikuwa ana mtoto wa wiki mbili,” amesema. Kamanda amesema polisi walipomtaka awaonyeshe mtoto, alidai kutokana na kazi anayofanya alilazimika kumzika ili aweze kuendelea na kazi yake. “Huyu binti anafanya kazi ya kuuza baa na kuuza mwili wake ku

Rais Samia: Chuo Cha Mwalimu Nyerere Kitasaidia Kuwaandaa Vijana

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kufunguliwa kwa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani, kutasaidia kuwaandaa vijana kuwa viongozi wazuri baadaye na kubadilisha mawazo na mitazamo yao ili kuisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo.   Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 23, wakati wa uzinduzi wa chuo hicho kinachomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi CCM ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa vyama sita rafiki vilivyopigania ukombozi katika nchi za Kusini mwa Afrika.   Ameongeza kuwa chuo hicho kitakwenda kufanya kazi ya tathimini ya maendeleo yaliyofikiwa kwenye nchi 6 zilizopigania uhuru katika nchi za kusini mwa Afrika na kwamba na kuangalia mwelekeo wa namna nchi hizo zitakavyosonga mbele kwa pamoja.

​Kajala Kupelekwa Mahakamani Baada ya Kumtosa Harmonize Kudaiwa Fidia Kwa Makosa Mawili

​Kajala Kupelekwa Mahakamani Baada ya Kumtosa Harmonize Kudaiwa Fidia Kwa Makosa Mawili MADAI yanayoendelea mitandaoni kuwa penzi la mwigizaji Kajala Masanja na msanii Rajab Kahali ‘Harmonize limevunjika limekaa vibaya kisheria. Endapo jambo hili ni kweli, Kajala anakabiliwa na hatari ya kupelekwa mahakamani kufunguliwa mashtaka kwa makosa mawili. Kifungu cha 69( 1 ) cha Sheria ya Ndoa iliyofanyiwa marekebisho 2010 kinasema kuwa mtu anaweza kufungua shauri na kudai fidia baada ya uchumba kuvunjwa. Ifahamike kuwa katika siku za hivi karibuni Kajala na Harmonize walijitangaza kuwa ni wachumba baada ya mwanaume huyo kumvisha pete mwanadada huyo, jambo ambalo linawaweka wawili hao katika hatari ya kufikishana kortini kidaiana fidia na zawadi. Kudai fidia na kurudisha zawadi ni vitu viwili tofauti ambavyo vyote vinaweza kumtia mmoja wa wachumba kwenye kasheshe ya kisheria. Kwa tafsiri rahisi fidia inahusu kulipwa maumivu aliyopata mmoja wa wachumba (mume au mke) kutokana na tukio hilo la ku

Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia kimya

Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia kimya 2 Machi 2022 CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Wanajeshi wa urusi walipovamia Crimea Mzozo wa Ukraine unaoendelea ukikaribia wiki moja sasa umeigubika siasa ya dunia. Wakati sehemu kubwa ya dunia ikionesha mshikamano na taifa hilo dhidi ya uvamizi wa jirani yake mkubwa, Urusi na mataifa mengi kuilaani Urusi, wanachojiuliza walimwengu ni kwa nini nchi nyingine zimekaa kimya Urusi na kiongozi wake Vladimir Putin wakiwekewa vikwazo vikali?. Nini kiko nyuma ya uamuzi wa kubakia kimya kwa nchi zenye nguvu kisiasa na kiuchumi katika kanda zao na duniani, kama vile Iran, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, India, China na Korea Kaskazini? Mchambuzi wa makala hii ana mtazamo ufuatao. Saudi Arabia na UAE Saudi Arabia na Urusi zinatajwa kama nchi mbili zenye nguvu zinazochimba mafuta na kwa pamoja zinatoa karibu robo ya mafuta yasiyosafishwa (ghafi) duniani. Saudi Arabia pia ni nguvu kubwa y

KALYNDA TAARIFA ILIYO JITOKEZA ZIDI YA KAMPUNI YA KALYNDA KUTO FUNGUKA APP YAO IMEFANYA

TAARUKI ILIYO JITOKEZA ZIDI YA KAMPUNI YA KALYNDA KUTO FUNGUKA APP YAO IMEFANYA WATU WALIYO JIUNGA KUWA NA PRESHA KWAKUWA MAMIA YA WATU WENGI WALIJIWEKEZA KATIKA APP IYO IITWAYO {Alunda au Kalynda} MAELEZO YA MAWASILIANO /Soma Zaidi Kuhusu/ Kuhusu Biashara ya Kielektroniki (Biashara ya Kielektroniki) Hatua ya kununua au kuuza bidhaa kielektroniki kwa kutumia huduma za mtandaoni kupitia Mtandao inajulikana kama e-commerce (au biashara ya kielektroniki). Biashara ya simu, uhamishaji wa fedha za kielektroniki, usimamizi wa msururu wa ugavi, uuzaji wa mtandao, usindikaji wa miamala mtandaoni, ubadilishanaji wa data wa kielektroniki (EDI), mifumo ya usimamizi wa orodha na mifumo ya kiotomatiki ya kukusanya data ni baadhi tu ya teknolojia zinazotumika katika biashara ya mtandaoni. Sekta kubwa zaidi ya tasnia ya umeme, biashara ya elektroniki inachochewa na maendeleo ya kiteknolojia ya sekta ya semiconductor. Fahamu kuhusu kalynda | Kalynda ni nini? Kalynda E-Commerce Co., Ltd. ni m

Sababu picha ya Rais, bendera kupandishwa Dubai hii hapa

Sababu picha ya Rais, bendera kupandishwa Dubai hii hapa WEDNESDAY MARCH 02 2022           Summary Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema kuwa bendera ya Tanzania kupandishwa kwenye jengo refu zaidi duniani la Burj Khalifa jijini Dubai ni zawadi kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Taifa. Dar es Salaam. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema kuwa bendera ya Tanzania kupandishwa kwenye jengo refu zaidi duniani la Burj Khalifa jijini Dubai ni zawadi kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Taifa. Juzi, ilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha bendera ya Tanzania ikiwa imefunika jengo hilo refu duniani lililopo Dubai. Leo Jumatano Machi 2, 2022 Dk Kijaji wakati akizungumzia mafanikio ya ziara ya Rais Samia aliyoifanya katika nchi za Ufaransa, Ubelgiji na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) amezungumzia suala hilo akisema hiyo ni moja ya mafanikio ya ziara hiyo. Amesema kuwa bendera hiyo ambayo ilipandishwa kwenye jengo refu kuliko yote du