Mabadiliko ya tabianchi ni tishio kwa binadamu na afya ya dunia , hatua zahitajika sasa:IPCC Ripoti © WMO/Kompas/Hendra A Setyawan Mwanamke akiwa amembeba mwanaye wakati wa mafuriko mjini Jarkata Indonesia 28 Februari 2022 Tabianchi na mazingira Ripoti mpya ya jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC iliyotolewa leo imesema kuchukua hatua sasa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kunaweza Kuchukua hatua sasa “Kunaweza kulinda mustakabali wetu kwani mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na shughuli za binadamu yanasababisha usumbufu wa hatari na ulioenea katika mazingira yetu na kuathiri maisha ya mabilioni ya watu kote ulimwenguni, licha ya juhudi zinazofanyika kupunguza hatari hiyo.” Wanasayansi wa jopo hilo wamesema katika ripoti kwamba “ Watu na mifumo duni ya ikolojia ndiyo ambayo haiwezi kustahimili na kuathirika zaidi. Ripoti hii ni onyo kali kuhusu matokeo ya kutochukua hatua," ameongeza Hoesung Lee, Mwenyekiti wa IPCC. Inaonyesha kuwa mabadiliko ya tabianchi