Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 24, 2022

Mzozo wa Ukraine na Urusi: Ukraine yawaambia raia wake waondoke Urusi, huku ikitangaza hali ya dharura

Mzozo wa Ukraine na Urusi: Ukraine yawaambia raia wake waondoke Urusi, huku ikitangaza hali ya dharura 23 Februari 2022 Imeboreshwa Saa 9 zilizopita CHANZO CHA PICHA, EPA Maelezo ya picha, Wanajeshi wa ziada wa Ukraine, wakifanya mazoezi ya kijeshi Ukraine pia inawakusanya wanajeshi wa ziada pamoja na wanajeshi wake wa kawaida kwa ajili ya kujiandaa kwa uwezekano wa uvamizi Baraza la kitaifa la usalama na ulinzi la Ukraine linafanya kazi kwa muda wa saa 24 kila siku na katibu wake mkuu amefanya mkutano na waandishi wa habari na kuwaambia kwamba Ukraine imeweka hali ya tahadhari. '' Hali ya tahadhari itawekwa katika nchi nzima ya Ukraine isipokuwa sehemu ya Donetsk na Luhansk'', amesema. Haya yanajiri huku, Urusi ikikabiliwa na mfumko wa bei ya mafuta na gesi huku mataifa hususan ya magharibi yakiiwekea vikwazo. MATANGAZO Hali ya tahadhari ina maanisha nini? Maandalizi ya kwanza yanaendelea katika kile ambacho Rais Zelensky alisema jana katika hotuba yake kwa taifa kwamb

TCRA yaeleza sababu ya bando kuisha haraka

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja vitu vitatu vinavyosababisha kuisha kwa bando haraka ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kasi ya internet, uwezo wa simu janja na kuwa na application nyingi kwenye simu Dar es Salaam.  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja vitu vitatu vinavyosababisha kuisha kwa bando haraka ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kasi ya internet, uwezo wa simu janja na kuwa na application nyingi kwenye simu. Pia imesema gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini ni nafuu ukilinganisha na nchi nyingine duniani. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jabiri Bakari ameyasema hayo jana Jumanne Februari 22 wakati wa mkutano wake na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF).  “Tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa, gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini Tanzania, zipo chini tofauti na nchi nyingine duniani, gharama za kawaida bila kujiunga na kifurushi, pamoja na gharama zilizounganishwa na ki

Absa Bank Yapongezwa kwa Juhudi za Utunzaji Mazingira

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai (kulia) akipokea moja ya miche iliyotolewa na Benki ya Absa kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Aron Luhanga (katikati). Kushoto ni Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Moshi Pendo Abdallah.     MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai ameipongeza benki ya Absa kwa mchango mkubwa inaotoa katika kuboresha mazingira hapa nchini ikiwemo mkoani humo. Kagaigai ametoa pongezi hizo jana (Jumatano) wakati akipokea jumla ya miche 2,100 ya miti ya asili kutoka kwa uongozi wa benki hiyo, katika ofisi za Mkuu wa Mkoa, zilizoko Moshi. “Kumekuweko juhudi kubwa zinazolenga kuboresha mazingira mkoani hapa, niwapongeze kwa mchango wenu huu muhimu na pia nitoe rai kwa taasisi zingine kuiga mfano wenu”, alisema. Aidha aliupongeza uongozi wa benki ya Absa kwa kutoa miche ya miti ya asili ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa utunzaji wa vyanzo vya maji. Mkuu wa Mkoa wa  Kilimanjaro,  Stephen Kagaigai akiotesha mti kama ishara ya kupokea msaada wa

TANESCO kuvuna bilioni 5 mapato ya mwezi kutoka GGML

Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa kupeleka umeme kwenye Kampuni ya Geita Gold Mining (GGML) ambao utaliwezesha TANESCO kupata kiasi cha Shilingi bilioni tano kwa mwezi zitakazotokana na mauzo ya umeme. Katikati ni Makamu wa Rais wa GGML, Simon Shayo.           KUKAMILIKA kwa mradi wa kupeleka umeme kwenye Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kunatarajiwa kutaliwezesha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupata kiasi cha Shilingi bilioni tano kwa mwezi zitakazotokana na mauzo ya umeme. Hayo yamebanika juzi tarehe 21 Februari, 2022 wakati wa shughuli ya utiaji saini mkataba wa mauziano ya nishati ya umeme baina ya TANESCO na GGML. Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika mjini Geita, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Maharage Chande amesema kuanza kwa biashara hiyo kutaiwezesha TANESCO kuongeza mapato yatakayosaidia kuboresha huduma mbalimbali kwa wateja wao. “Maana ya pili tutapunguza uzalis

Madalali Kariakoo Auction Mart Watifuana, Wawapandisha Kizimbani Viongozi Wao

Mmoja wa madalali akionesha nyaraka walipokuwa wakizungumza na wanahabari.     MADALALI wa Kariakoo Auction Mart wametifuana na uongozi wao wakiwatuhumu viongozi hao kukaa madarakani kwa zaidi miaka saba bila kufanyika uchaguzi wa kupata viongozi wapya wakati katiba yao inasema uongozi unatakiwa kukaa madarakani miaka mitatu na kufanyika uchaguzi. Huyu naye akitoa malalamiko yake.     Madalali hao wamesema kilio chao kikubwa kwa uongozi huo licha ya kukaa madarakani muda mrefu wamekuwa hawana maendeleo kwenye umoja wao huo. Wakiendelea kuwatuhumu viongozi wao madalali hao wamewaomba viongozi mbalimbali wa serikali kufika kwenye ofisi yao na kuangalia mazingira wanayofanyia kazi ili wajionee wenyewe. Sehemu ya choo wanachotumia na kuwalalamikia viongozi kwa mazingira hayo duni.     Hata hivyo wanahabari wetu waliutafuta uongozi wa madalali hao na kufanikiwa kuzungumza na Katibu wao aliyejitambulisha kwa jina la Swalehe Omari Msoka ambaye alikiri uongozi wao kukaa madarakani kwa zaidi ya

TMA Yatoa Angalizo La Mvua Kubwa

MAMLAKA  ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa angalizo la mvua kubwa kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, Pwani ikijumuishwa na visiwa vya Mafia, Ruvuma, Morogoro, Njombe, Lindi na Mtwara itakayonyesha hii leo Februari 23, 2022.   TMA imesema kuwa kutakuwa na upepo mkali katika maeneo ya ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, na Tanga.   Aidha, TMA imeongeza kuwa mvua itaendelea kunyesha kwa siku mbili zijazo kwa baadhi ya mikoa nchini Tanzania.

Rais Samia: Chuo Cha Mwalimu Nyerere Kitasaidia Kuwaandaa Vijana

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kufunguliwa kwa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani, kutasaidia kuwaandaa vijana kuwa viongozi wazuri baadaye na kubadilisha mawazo na mitazamo yao ili kuisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo.   Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 23, wakati wa uzinduzi wa chuo hicho kinachomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi CCM ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa vyama sita rafiki vilivyopigania ukombozi katika nchi za Kusini mwa Afrika.   Ameongeza kuwa chuo hicho kitakwenda kufanya kazi ya tathimini ya maendeleo yaliyofikiwa kwenye nchi 6 zilizopigania uhuru katika nchi za kusini mwa Afrika na kwamba na kuangalia mwelekeo wa namna nchi hizo zitakavyosonga mbele kwa pamoja.