Fahamu umuhimu wa ziara ya Rais Samia Ulaya kwa Watanzania Beatrice Kimaro Mchambuzi, Tanzania Saa 4 zilizopita CHANZO CHA PICHA, IKULU MAWASILIANO Maelezo ya picha, Siku 10 za ziara aliyoifanya Rais Samia hivi karibui zimefungua milango ya mahusiano ya kidiplomasia, kiuchumi na kijami "Tanzania itakuwa sawa na Ulaya ndani ya miaka 6", hii ilikuwa kauli ya Rais wa taifa hilo, Samia Suluhu Hassan mara baada ya kurejea nyumbani mwishoni mwa wiki akitokea barani Ulaya alikokuwa na ziara ya kikazi katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji. Ni kauli iliyoibua mjadala mkubwa. Wapo wanaojiuliza itawezekanaje? Na wapo wanaoona inawezekana. Lakini hilo halizuii mtazamo wa namna ziara hiyo ilivyoleta sura tofauti kwenye nyanja ya kidiplomasia na fedha za maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Siku 10 za ziara hiyo zimefungua milango ya mahusiano ya kidiplomasia, kiuchumi na kijami, milango ambayo ilifungwa kwa 'kufuli la chuma' katika kipindi cha utawala