Wananchi Tanzania walalamika na kupinga viwango vya Bima ya afya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi wakati wa kikao na wakurugenzi wa wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya Tanzania. Wananchi wameilalamikia Serikali ya Tanzania na kupinga hatua ya Wizara ya Afya kupendekeza viwango vya kulipia Bima ya afya ambavyo ni Sh. 340,000 kwa kaya ya watu 6 na Sh. 84,000 kwa mtu mmoja asiye na familia katika kipindi cha mwaka mmoja. Kiwango hicho kinapigwa vita na wananchi walio wengi kutokana na hali ya ngumu ya maisha nchini humo. Ingawaje kwa muda mrefu ni wananchi wachache nchini Tanzania ndiyo wenye uhakika wa matibabu kwa kuwa na bima ya afya huku asilimia 85 ya wengine wakikosa huduma hiyo. Hata kulingana na takwimu hizi, Serikali imeshindwa kuwakomboa wananchi wake kwa kupendekeza viwango rafiki vitakavyopelekea kila mwananchi kuweza kulipia bima hiyo bila usumbufu wowote. Zuberi Mkalaboko Mkazi wa Morogoro amesema viwango vilivyopendekezwa na Wizara havitawasaid